Kero za kivuko cha Feri. Matatizo na suluhisho

 1. Huduma ya kivuko kati ya Kigamboni na Kivukoni(Ferry) inalalamikiwa sana na wananchi hususan wakazi wa Kigamboni.
  Huduma ya kivuko imekuwa sio ya uhakika, hakuna usalama na pia vyombo hutumia muda mrefu majini kwa safari moja (Safari moja ilitakiwa kutumia dakika 15-20, lakini Safari hiyo kwa sasa inachukua zaidi ya sana moja au zaidi).

Nini chanzo za changamoto hizi:

 1. Uchakavu wa pantoni zilizopo za MV Kigamboni na MV Magogoni. Pantoni hizi hazijafanyiwa matengenezo makubwa kwa muda mrefu sasa. Kila pantoni ina injini nne lakini si zote zinafanya kazi. Miili ya vivuko ina kutu na milango imepinda.
 2. Ufinyu wa maeneo ya kuingia na kutokea kwenye kivuko. Kwa upande wa Kivukoni, barabara ya kutokea na kuingilia kwenye kivuko ni finyu sana, imebanwa na masoko ya samaki, kituo cha mabasi ya DART, kituo cha mabasi ya UDA na Taxi. Vile vile kufungwa kwa Barabara ya Barack Obama  eneo la Ikulu nako kunachangia kuleta msongamano. Kwa upande wa Kigamboni, barabara ya kuingilia na kutokea  kwenye pantoni ni finyu. Magari yanayoingia na kutoka kwenye kivuko yanapishana kwa tabu. Vile vile shughuli za kibiashara, Bajaj na pikipiki navyo vinasababisha msongamano.
 3. Vyumba vya kusubiria abiria ni vidogo sana hususan kwa upande wa Kigamboni. Wananchi wanapata usumbufu mkubwa vipindi vya asubuhi na jioni waendapo na kutoka kazini.
 4. Uwingi wa wasimamizi. Katika kivuko hhiki kuna watumishi wa TEMESA, Askari Polisi, SUMA JKT, Polisi wa Jeshi (Military Police). Kila moja hawa anafanya lake. Wako bize kupitisha “abiria wao na magari yao”. Askari na wasimamizi hawa hupokea fedha na malipo haya hayaingii kwenye mfuko wa Serikali. Utaratibu huu wa wasimamizi wengi unasabisha usumbufu usio na lazima kwa wananchi.
 5. Ukataji wa tiketi sio mzuri. Kuna na msongamano mkubwa hususan wakati wa asubuhi.
 6. Morali ipo chini kwa watumishi wa TEMESA. Uongozi wa juu wa TEMESA hauwajali watumishi wake. Wanalalamika sana. Zaidi ya 80% ya watumishi wa huduma za kivuko wana mikataba ya muda mfupi ya kati ya 1-3. Nahodha mwenye dhamana ya kuendesha chombo analipwa Tsh 350,000 kwa mwezi na wanafanya shift ndefu hadi  masaa 12 kwa siku. Hali hii imepelekea kwa huduma hii kuhujumiwa. Hujuma ni pamoja na watumishi kwa makusudi kukamisha vivuko mchangani, kuendesha vivuko kwa injini mbili badala ya nne, kuchelewesha safari na kuuza mafuta kwa wavuvi
 7. Uongozi wa TEMESA kushindwa kuwajibika na kusimamia majukumu yake kikamilifu. Wameshindwa kuboresha huduma za kivuko. Wameshindwa kusimamia matengenezo ya vivuko. Wameshindwa kusimamia maslahi ya watumishi. Wameshindwa kusimamia mapato (takribani ya Tsh 5 milioni inapotea kila siku).

Nini kifanyike?

 1. Kuwepo na mpango mahsusi wa kufanya matengenezo ya vivuko hivi. Matengenezo yaanze baada ya daraja la Kigamboni kufunguliwa. Aidha, kitafuywe  kivuko cha muda kuziba pengo la kivuko kitakachopelekwa matengenezo. Vile vile, ununuzi wa pantoni mpya uharakishwe.
 2. Upanuzi wa miundombinu ya Barabara za kuingia na kutokea kwenye kivuko unahitajika. Hili liende sambamba na upanuzi wa sehemu za kusubiria abiria.
 3. Kwa kipindi cha mpito mabasi ya UDA yatumie vituo na barabara za UDART. Pindi mradi wa DART utakapoanza, mabasi ya UDA yahamishiwe kabisa pale Kivukoni na kupelekwa sehemu nyingine ambako hakuna mfumo wa DART.
 4. Mfumo wa kukata tiketi na kuingia kwenye kivuko uwe wa kielektroniki. Kuwe na tiketi za siku na za msimu. Kuna watu wanavuka kila siku, kwa nini awe anakata tiketi kila siku? Kwa nini kusiwe na tiketi wiki au mwezi?
 5. Mfumo wa usimamizi kwenye kivuko unahitaji kuangaliwa upya. Walinzi wa TEMESA, SUMA JKT, Polisi na MP wa Jeshi wote wanafanya kazi gani? Kwa maslahi ya nani? Hawa ndio wanasababisha kero na ndio mwanya wa upotevu wa mapato.
 6. Maslahi na mikataba ya watumishi wa TEMESA iangaliwe upya. TEMESA nayo inahitaji kujipanga upya baada ya mabadiliko ya uongozi hivi karibuni.

Tunashukuru kwa hatua zilichokuliwa na Waziri Makame Mbarawa kwa kubadilisha uongozi wa TEMESA. Tunashukuru pia kwa Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kufanya ziara ya kushtukiza. Naamini kilio chetu kimefika na mapendekezo haya  yatafanyiwa kazi. Wananchi wanataka kuona huduma ya kivuko iliyo bora, salama na ya uhakika.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized and tagged , , , . Bookmark the permalink.

4 Responses to Kero za kivuko cha Feri. Matatizo na suluhisho

 1. olive says:

  Kwa kweli binafsi nimetokea kuichukia kigamboni kutokana na kero hii. Na nina mpango wa kuhama labda nitarudi miundombinu itakapokaa sawa.

  Like

 2. Kapongoliso says:

  Daraja lizinduliwe tu ili hawa TAMESA waachiwe hicho kivuko chao maana tumechoka sasa.

  Like

 3. mhando says:

  kaka yote uliyoongea ni ukweli mtupu..wananchi tumekua hatuna haki na kivuko kila gari linalo pita ni staf sasa ushauli wangu waweke kibao kabisa tujue kivuko wananchi hakiwausu.umeongelea waenda kwa miguu wanatumia saa nzima je wenye magari..mm mpaka najiona kama naishi mbagala au kongowe kwa kuzunguka.kaka ww tumekuchagua utuondolee hizi kadhia nawe ni mzaa haswa jitahidi.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s