Tatizo la msongamano. Nini kifanyike?

Kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya mwaka iliyoanzisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeainisha moja ya majukumu ya taasisi hii ni kuwa hospitali ya rufaa ya Taifa.

Taasisi hii ina uwezo wa kulaza wagonjwa 1500 (bed capacity).  Takwimu zilizopo kwenye tovuti ya taasisi hii zinaonyesha kuwa hospitali hii inapokea wagonjwa wa nje (outpatients) wapatao 1000-2000 kwa siku na wanalaza wagonjwa 1000-1200 (inpatients) kwa wiki.

Kwa muda mrefu tumeshuhudia hospitali hii kuzidiwa na wagonjwa. Wagonjwa wengi wakiwa ni wagonjwa ambayo wangeweza kutibiwa kwenye hospitali za pembezoni. Hali ambayo imesababisha msongamano na baadhi ya wagonjwa kulala chini.

Kumekuwa na kauli kuwa msongamano wa Muhimbili unatokana na huduma za afya zinazotolewa kuwa nzuri. Hoja hii sio sahihi sana. Tatizo la msongamano katika hospitali ya Muhimbili ni la kimfumo. Pamoja na juhudi za Mhe. Rais la kutaka kuondokana na wagonjwa kulazwa chini, bado ongezeko la vitanda halitaondoa matatizo ya msingi. Vitanda vitajaa na bado mahitaji ya vitanda vya ziada yataendelea kuwepo.

Matatizo ya kimfumo ya msongamano ni yapi?

  1. Mfumo wa rufaa in dhaifu. Hospitali ya Muhimbili ilipaswa kupokea wagonjwa ambao wameonwa kwenye hospitali za pembezoni na ambao wanahitaji vipimo au matibabu mahsusi ambayo hayapatikani kwenye hospitali hizo. Kinyume chake, wagonjwa wenye magonjwa ya kawaida ambayo yangeweza kutibiwa pembezoni na kina mama wenye ujauzito usio na matatizo ndio waliojaa Muhimbili. “Chujio” la kuwachuja wagonjwa halipo. Kwa mfano, kuna vituo vya Afya vya Mnazi Mmoja, Ilala na Round Table, Mbagala ambazo zina huduma za msingi za uzazi lakini havitumiki kikamilifu badala wagonjwa wake kupelekwa Muhimbili.
  2. Hospitali na vituo vya Afya vya pembezoni kutokuwa na vifaa and wataalamu wa kutosha-Huduma za Amana, Mwananyamala, Temeke, Rangi Tatu na Vijibweni zilipaswa kuwa vyumba vya upasuaji, vyumba vya kuzalia, vifaa na wataalamu kutosha. Hakuna sababu za msingi kwanini mwanamama atoke PembaMnazi, Kivule, Mabwepande au Chamazi akajifungulie Muhimbili. Hata pale ambapo vifaa vipo na madaktari wapo mzigo husukumiwa Muhimbili. Tujiulize not operesheni ngapi za uzazi (Caesarean section) zinazofanyika kwenye hospitali hizi za pembezoni ukilinganisha na Muhimbili? 
  3. Kutokuwepo na mfumo mzuri wa mawasiliano na uratibu kati ya TAMISEMI na Wizara ya Afya. Hospitali ya Muhimbili na za rufaa ziko chini ya Wizara wakati zahanati, vituo vya afya, hospitali za Wilaya na Mkoa ziko chini ya TAMISEMI. Kila Wizara inafanya mambo yake bila kuwa na mawasiliano na uratibu wa pamoja. Tatizo la msongamano linasababishwa na Tamisemi kutowajibika kikamilifu. Idara ya Afya ndani ya TAMISEMI bado ni ndogo sana kuweza kuratibu huduma za afya. Kuna mjadala ndani ya Wizara ya Afya wa kutaka kurudisha hospitali za mikoa Serikali. Kwangu, hili sio suluhisho. Tutibu mfumo na sio kutengeneza mfumo mbadala.

Nini kifanyike?

  1. Mfumo wa rufaa upitiwe upya na kuimarishwa. Kuwe na vigezo vya kumpatia rufaa mgonjwa kwenda Muhimbili.
  2. Hospitali za pembezoni zijengewe uwezo na kupatiwa Vifaa na wataalamu ili waweze kushughulikia wagonjwa na upasuaji usio na “complications”. Jiji la Dar Es Salaam linakuwa kwa kasi sana, Wizara ya Afya na TAMISEMI zianishe maeneo ya kimkakati ya kujenga vituo vya Afya na hospitali. Kwa mfano, Katika Wilaya ya Kinondoni katika njia ya kuelekea Bagamoyo, zaidi ya hospitali binafsi zaa Rabinisia, Massana na hospitali ya Jeshi Lugalo hakuna kituo kikubwa au  hospitali ya umma. Tuangalie huduma za Afya kimkakati.
  3. Mfumo wa mawasiliano na uratibu wa huduma za Afya uboreshwe na kusimamia vizuri.

Hitimisho

Bila ya kuliangalia tatizo la msongamano kimfumo tutamaliza ofisi zote za umma na bado wagonjwa wataendelea kulala chini.  Tuelekeze juhudi zetu katika kurekebisha mfumo na tatizo la msongamano litapungua.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s