Kituo cha matibabu ya dawa za kulevya, Vijibweni, Kigamboni

image
Leo jioni nilialikwa kwenye kituo cha matibabu ya madawa ya kulevya kilichopo Vijibweni katika Jimbo la Kigamboni. Pichani nikiwa na vijana walio kwenye hatua mbalimbali za matibabu. Kituo hiki kinaongozwa na watumiaji wa madawa ya kulevya waliopona. Bibie mwenye ushungi ni mmoja wa viongozi wa kituo hiki. Naye alikuwa ni mtumiaji wa madawa ya kulevya aliyepona. Niliweza kupata ushuhuda wa kusisimua kuhusu maisha ya uteja.
image
Nyuso za furaha. Nami nilifarijika kuona vijana hawa wamejitambua na kuamua kuacha kutumia madawa ya kulevya.
image
Leo ilikuwa ni siku ya kipekee kwa kijana huyu ambaye ametimiza mwaka mmoja bila kutumia madawa ya kulevya.
Kijana huyu alinisimulia maisha yake katika uteja. Alinieleza jinsi alivyoanza, jinsi alivyoishi maisha ya uhalifu ili kumudu gharama za uteja na jinsi alivyokata shauri kurudi kwenye mstari.
Nikiwa kama Mbunge na pia Daktari niliwashauri na kuwapa moyo kwenye safari yao ya matibabu yenye hatua 12 (12 Steps).

Tanzania bila ya madawa ya kulevya inawezekana!

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized and tagged , , , , , . Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s