Mtazamo wangu juu ya uteuzi wa Makatibu Wakuu Wapya

Hatimaye uteuzi wa makatibu wakuu uliokuwa unasubiriwa kwa hamu umefanyika jana tarehe 21 Agosti 2013. Baadhi ya Wizara zilikuwa na makaimu katibu wakuu kwa muda mrefu baada ya waliokuwepo kuondolewa madarakani au kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Kwa ujumla nimefurahishwa na uteuzi huu kwani wengi waliopata nafasi ni wachapakazi na wenye sifa za kutosha kupata nafasi hizi.

Kwa mfano, sekta ya afya imepata katibu mkuu mpya. Ujio wa Bw Charles Pallangyo toka ofisi ya Waziri Mkuu utaleta mtazamo mpya ndani ya Wizara. Vile vile nimefurahi kuona Dkt Donan Mmbando akithibitishwa katika nafasi ya Mganga Mkuu Wa Serikali. Ni kijana na uwezo mkubwa katika utendaji. Ili waweze kufanya vizuri zaidi wanahitaji wakurugenzi wa idara ambazo nyingi bado zipo wazi.

Nimefurahi pia kuona Bw Jumanne Sagini amekuwa katibu mkuu kamili Tamisemi. Amekuwa aki kaimu nafasi hii kwa muda mrefu na kazi yake ilikuwa nzuri. Vile vile uteuzi wa Zuberi Samataba kama Naibu Katibu Mkuu (Elimu) ni chaguo zuri. Ni kijana na mwenye uelewa mzuri wa sekta ya elimu. Ninaamini atakuwa na mchango mkubwa katika sekta hii. Nimefurahi pia kuona sekta ya afya imepewa kipaumbele katika Tamisemi. Sekta hii nyeti na muhimu ilikuwa na kitengo kidogo ndani ya Tamisemi. Uteuzi Wa Dkt Deo Mtasiwa ni chaguo zuri. Ni hazina kubwa iliyokumbwa na “ajali katika kazi”. Ana ufahamu mzuri wa sekta ya afya na ninaamini atakuwa na mchango mkubwa katika katika kuimarisha mifumo ya afya katika Tamisemi na kujenga mahusiano mazuri na Wizara yake ya zamani ya afya.

Wizara ya Ardhi nayo imepata katibu mkuu na naibu mpya. Wizara hii nayo ina changamoto nyingi.
Simfahamu Katibu Mkuu mpya Bw Alphayo Kidata ila msaidizi wake Dkt Selassie Mayunga alikuwepo hapo Wizarani kama Mkurugenzi wa upimaji na ramani. Bw Kidata bado ana kazi kubwa ya kusafisha uozo ndani ya Wizara hii na kurejesha imani ya wananchi kwa watendaji wa wizara hii. Nitumie nafasi hii kumtakia Bw Patrick Rutabanzibwa mapumziko mema. Pamoja na changamoto zote na maneno yanayosemwa dhidi yake, binafsi ninaona alifanya kazi nzuri.

Wizara ya Elimu na Ufundi, imepata katibu mkuu na naibu katibu mkuu mpya. Nimefanya kazi kwa muda mfupi na Prof. Sifuni Mchome wakati nikiwa Makamu wa Mwenyekiti Wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. Ni mchapakazi na nina imani atatoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu ambayo kwa sasa inakabiliwa na changamoto nyingi. Akiwa mtendaji mkuu wa TCU ameweza kuleta mabadiliko makubwa. Vilevile alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Waziri Mkuu iliyochunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne. Ninaamini atatumia fursa hii kuitoa hadharani ripoti hii na kufanyia kazi mapendekezo aliyoyatoa yeye mwenyewe. Sekta hii inahitaji maboresho makubwa.

Ninawapongeza pia, Bi Regina Kikuli, mama mchapakazi na anayejituma. Nimefanya naye kazi kwa karibu Wizara ya Afya wakati nikiwa katika utumishi wa umma. Anastahili uteuzi huu. Vile vile nampongeza mjumbe mwenzangu kwenye Bodi za MNMA na MSD, Bi Monica Mwamunyange ambaye alikuwa ni Kamishna wa Bajeti. Ana uelewa mkubwa wa masuala ya fedha na bajeti. Namtakia kila la kheri katika majukumu mapya ndani ya Wizara ya Uchukuzi. Natumai atakwenda vizuri na kasi ya Waziri Harrison Mwakyembe. Wizara hii ina taasisi nyingi zilizooza.

Mwisho, kwa mtazamo wangu uteuzi huu ni mzuri. Cha msingi makatibu wakuu hawa tuwape nyenzo na ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao vyema kwa Ustawi wa nchi yetu.
Nimeanza kuona maandiko kwenye mitandao ya kuwabeza na kuwashambulia baadhi yao. Tuwape nafasi na baada ya muda tuwafanyie tathmini ya utekelezaji Wa majukumu yao. Ni mapema sana kuanza kuwashambulia na kuwabeza.
Nawatakia kazi njema.

Dkt Faustine Ndugulile
Mbunge Wa Kigamboni

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized and tagged , . Bookmark the permalink.

2 Responses to Mtazamo wangu juu ya uteuzi wa Makatibu Wakuu Wapya

  1. Perfect observation

    Like

  2. Senga Sembuche says:

    Mheshimiwa it seems like you are familiar with some of these people well and are confident about them, however to help some of us have the same level of trust as you do in them and the government in general, it could help if you mention specifically how their leadership made a difference i the positions they previously held, what did they achieve, what is their style of leadership and so forth..even just briefly.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s