Kodi ya sim card: Kupanga ni kuchagua

Kwa takribani wiki mbili sasa kumekuwa na mjadala mkubwa kwenye vyombo ya habari na mitandao kuhusu kodi ya kadi za simu (sim card tax). Malalamiko haya yamelenga kuonyesha kuwa kodi hii haifai na gandamizi hasa kwa wananchi wa kipato cha chini na kwamba kodi hii ifutwe.

Kodi hii ilipitishwa na Bunge la Bajeti ambalo limeisha mwezi Juni, 2013. Ingawa sikuwepo  siku suala hili linajadiliwa, katika uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) nami kama mbunge ni sehemu ya maamuzi haya, siwezi kukwepa.

Nianze kwa kuwapongeza wale wote walioshiriki kuipigia kelele kodi hii na kuhamasisha jamii kuhusu kupinga kodi hii. Wamefanya kampeni za kiistarabu bila vurugu wala matusi, na kikubwa zaidi wametumia vizuri mitandao ya kijamii katika kuhamasisha jamii na kukusanya saini za wanaopinga kodi hii.

Namshukuru Mheshimiwa Rais naye kwa kusikia kilio hiki na kuamua kukifanyia kazi. Binafsi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana kampeni hii. Kitu moja kilichokosekana kwenye kampeni hii ni ushawishi kwa nini kodi hii ifutwe. Nilitarajia wahamasishaji wataueleza umma kwa nini wanadhani kodi hii ni gandamizi; nini athari ya kodi katika matumizi ya simu, makampuni ya simu na uchumi wa nchi kwa ujumla. Matumizi ya takwimu yangesaidia sana kujenga hoja.

Tukumbuke kuwa kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusiana na huduma ya umeme nchini. Katika mijadala mingi wakati wa Bunge la Bajeti, wabunge wengi walitaka Serikali itoe kipaumbele katika kusogeza huduma za umeme vijijini.

 Ili kufanikisha azma hii Serikali ilihiitajika kubuni mikakati mipya ya kupata vyanzo vya mapato kwa ajili ya huduma hii na bajeti nyingine za maendeleo.

Lengo la kodi ilikuwa ni kukusanya kiasi cha Tsh 170 Billioni. Hivyo kwa kuifuta kodi hii, Serikali itabidi itafute vyanzo mbadala wa kuziba pengo hili ambalo si dogo.

Inawezekana, hakuna utafiti wa kutosha uliofanyika kabla ya kuanzisha kodi hii. Inawezekana pia, sisi wabunge hatukuiangalia kwa mapana kodi hii. Kodi hii ilipitishwa na Bunge, itabidi irudi tena Bungeni kufanyiwa mapitio.

Kuna mambo mawili yanaweza kufanyika. Moja, ni kuifuta kabisa kodi hii au kodi hii kufanyiwa maboresho. Moja ya maboresho ni kutoza kodi hii kwa uwiano wa kipato au matumizi ya simu. Njia nyingine ni kutoza kodi ndogo kwa watumiaji wa pre-paid na kutoza kodi kubwa kwa watumiaji wa Post-paid ambao wengi wana kipato kikubwa na wengine kulipiwa na taasisi wanazotumikia.

Nitaendelea kufuatilia kwa karibu mapendekezo yatakayoletwa Bungeni na Serikali juu ya kodi hii. Vilevile ningependa kuona hoja zenye ushawishi kutoka kwenye jamii kwa nini kodi hii ifutwe.

Je tupo tayari kuendelea kuona 15% ya watanzania wakiwa na huduma ya umeme pekee? Je tupo tayari kuendelea kuona wananchi waishio vijijini wakiishi bila umeme? Je kodi ya kadi ya simu ina athari gani katika kipato na maisha ya moja kwa moja ya mwananchi? Je ni vipi pengo hili katika bajeti litazibwa?

Kupanga ni kuchagua. Kwenye wengi haliharibiki neno. Ninaamini tutakuwa na mjadala mpana na mwisho maamuzi sahihi kufanyika.

Mwisho niwasihi wanasiasa wenzangu kutotumia hoja hii kujitafutia umaarufu binafsi na kuleta ushabiki wa kisiasa.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized and tagged , , , , . Bookmark the permalink.

One Response to Kodi ya sim card: Kupanga ni kuchagua

  1. Hassan Ninga says:

    Mie naona hapakufanyika utafiti wa kina kuhusu hili jambo naweza kusema kuna kukurupuka hakuna elimu mpaka sasa iliyotolewa hata watu wa mitandao kuhusu kodi hiyo mie siungu mikono hilo
    Tz tuna vyanzo ving vya mapato tuna madin ya tanzanite ambayo dunia nzima yanapatikana kwetu ,mbuga za wanyama ,bandari haya na gesi hiyo tatizo n vya wachache

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s