Utatuzi wa uvunaji wa gesi Mtwara bado kitendawili. Chanzo ni nini?

Nimepokea taarifa za kushtusha kuhusu vurugu zilizotokea au zinazoendelea huko Mtwara kuhusu kupinga gesi iliyovumbuliwa mkoani hapo kupelekwa Dar Es Salaam kwa ajili ya nishati ya umeme.

Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa, watu kadhaa wameuwawa na mali kuchomwa moto au kuharibiwa.

Hapo nyuma, nilishwahi kuandika kuhusu tatizo hili na kutoa tahadhari. Bofya hapa kusoma zaidi.

Pamoja na juhudi za Serikali kupitia Waziri Mkuu kulishughulikia tatizo hili, naona bado suluhu bado kupatikana.

Mimi kama Daktari , mgonjwa anapokuja na homa, huwa sitibu homa au kujaribu kushusha ile homa, huwa najikita zaidi katika kutafuta chanzo cha homa. Unapotibu chanzo, homa hutoweka kabisa. Inawezekana kabisa wakati wa kushughulikia suala hili Serikali imekuwa inashughulikia dalili za homa bila kutafuta chanzo cha homa.

Katika mada hii nitajaribu kuja baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa kiini cha tatizo hili.

 1. Kuna taarifa ya mvutano mkali wa kisiasa hususan kwenye Chama tawala cha CCM katika Mkoa wa Mtwara. Mvutano huu unatokana kambi na makovu ya uchaguzi wa mwaka 2010. Je inawezekana vurugu na uchochezi kuwa unafadhiliwa na  makundi haya hasimu?
 2. Je inawezekana kuwa kuna mkono wa vyama pinzani vya siasa wenye lengo la kukwamisha mradi huu au kujitafutia umaarufu wa kisiasa?
 3. Kumekuwa na ongezeko la wanaharakati ambao wanawasapoti wananchi katika suala hili. Je wanaharakati hawa ni kina nani? Nini malengo yao? Nani wako nyuma yao?
 4. Mradi huu unagharimu fedha nyingi sana. Taarifa zilizopo ni kuwa gharama za mradi ni mara 3-4 ya gharama za halisi za ujenzi wa bomba kama hili. Je kuna vita ya kimaslahi kati ya wale waliopata tenda na wale waliokosa? Je nani atanufaika na mradi huu?
 5. Kwa kuwa mradi huu ni wa fedha nyingi, inawezekana makundi ndani ya chama tawala yenye malengo ya uchaguzi 2015 yakawa katika vita ya kutaka kuwamisha mradi huu. Kwani ushindi wa kundi moja utawezesha kundi kupata fedha “kulishughulikia” kundi jingine. Je tumeliona hili?
 6. Kuna suala la ushindani wa biashara katika makampuni ya kimataifa. Je kuna uwezekano wa vurugu kuratibiwa na makampuni yaliyokosa tenda au yale yanayoshindana kibiashara?
 7. Je inawezekana vurugu hizi zina mkono wa Serikali au vikundi toka nje vyenye malengo ya kutibua amani na utulivu nchini, kwa malengo ya kibiashara? Je tumefanya utafiti kuhusu jambo hili?
 8. Mkoa wa Mtwara kama ilivyo mikoa mingi ya kusini ipo nyuma sana kimaendeleo.  Kwa mtazamo wa wananchi hawa, wanaona kwamba wamesahaulika na hawakumbukwi kwenye miradi ya maendeleo. Pia kuna kundi kubwa la vijana ambao wanaishi katika hali ya umaskini na kukosa matumaini. Uvumbuzi wa gesi unaonekana kama mkombozi mkubwa katika kunyanyua hali yao ya kiuchumi. Je wananchi hawa wamepewa elimu ya kutosha? Je faida za mradi zimeelezwa kwa ufasaha kwa wananchi hawa? Je wananchi hawa wameshirikishwa kikamilifu? Kwa kuwa wananchi hawa wamekuwa wakipewa ahadi nyingi huko siku za nyuma, je wana uhakika gani kuwa mradi huu wa gesi utakuwa na manufaa kwao?

Moja au mambo yote niliyoelezea hapo yanaweza kuwa ni chanzo cha vurugu tunazoziona huko Mtwara.

Suluhu ya jambo si matumizi ya nguvu na kubeza. Suluhu ya jambo ni kutumia hekima na busara. Suluhu ya jambo ni kusikiliza na kujua hoja zinazopelekea wananchi kupinga jambo hili. Suluhu ya jambo hili ni kufanya utafiti wa kina kujua kiini na kushughulikia tatizo hilo kikamilifu.

Bila kujua kiini, tatizo hili halitaaisha wala kuondoka.

Mwisho, napenda kutoa pole kwa familia za wale waliofiwa, walioumia na kuharibiwa mali zao.

Tanzania imekuwa ni nchi ya amani na utulivu, sote tuna wajibu wa kulinda amani hii na kuidumisha.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized and tagged , , , . Bookmark the permalink.

4 Responses to Utatuzi wa uvunaji wa gesi Mtwara bado kitendawili. Chanzo ni nini?

 1. Felix says:

  umemaliza vizuri sana, suluhu ni kukaa na wananchi kwa kuwa wamekuwa wakionekana wako nyuma kimaendeleo hivyo ni rahisi kwao kuona serikali ina wabeza na ndio wanaamua kutumia njia hii ya vurugu. Sidhani kama wananchi hawa hawaambiliki au hawana upeo wa kutafakari mapendekezo ya serikali

  Like

 2. Maswali yote nane ndio jibu la tatizo, na yote yanatakiwa yawe adressed. Issue ya Mtwara ina Political will na pia ina finances behind it. Execution yake inaoneka wazi kuwa ni mpango uliojitosheleza.Tangia hizi vurugu zimeanza Mheshimiwa Rais amewaachiwa wadau wengine wakatatue kwa niaba yake, Ila ninaona huu ni wakati wa Kiongozi wa Nchi kwenda huko.

  Cha kuangali ni kitu kimoja tu? Je issue ya Gesi Kishizimwa, Isuues ya Dini itaibuka tena, Maanda mimi ni muunini wa Trend Analysis, na nimefanya uchunguzi wangu nimegundua hizi issue Mbili zinapokezana. Na imani yangu ni kwamba, either both project za Udini/Mtwala viko executed na mtu mmoja or Makumbi mawili yanayopingana.

  Cha msingi kuliko vyote, Tunaomba serekali iwaonyeshe wabunge huo mkataba, Hamna haja ya kuuficha ficha, hata kama watoneshwa chini ya kiapo maalumu hiyo itasaidia sana.

  At the end of the day, Tunataka Amani na maendeleo.

  Like

 3. Apollo Temu says:

  There are PLENTY lessons on what works and what NEVER works from various spots in the world where this high profile resource always brings contention! There are PLACES where this resource BRINGS and enhances PEACE and PROSPERITY ! Key here is effective and lasting stakeholder management from DAY 1! There are NO short cuts and lest be a different avenue at our own peril!

  Like

 4. Apollo Temu says:

  The IRONY is, the abundance of resources here is sufficient for EVERYONE, and EVERY player to be FULLY satisfied in terms of benefits from the richness ! The only show stopper between where we are and to the achievement is GREED and IGNORANCE!

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s