Changamoto ya Gesi ya Mtwara ishughulikiwe haraka

Hivi karibuni baadhi wa wananchi wa mkoa wa Mtwara waliandamana wakidai kuwa gesi iliyovumbuliwa ibaki mkoani hapo badala ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Hapo mwanzoni, suala hili ilonekana kuwa ni dogo lakini kadri muda unavyokwenda, badala ya kuwa kipele kinaekelea kuwa jipu na mwisho kinaweza kusababisha kansa itakayosambaa mwili mzima.

Nimefuatilia kwa makini kuhusu hoja ya wananchi wa Mtwara lakini vile vile nimefuatilia kwa makini majibu yanayotolewa na viongozi mbalimbali. Kinachoonekana ni kwamba, viongozi hawajipanga vizuri. Kila mtu anasema lake na kila mtu anafanya lake.

Kwa mtazamo wangu, katika sakata hili kuna mambo mawili makubwa ya msingi. Mosi, maendeleo duni katika mikoa ya Kusini ikiwa ni pamoja na Mtwara. Pili, tatizo la ajira vijana.

Haya ndio mambo ya msingi. Kinachohitajika ni kutoa elimu ya kutosha itakayolenga kuwashibisha wananchi wa Mtwara jinsi gani watanufaika kimaendeleo na kwa upande wa ajira kwa vijana.

Kubeza na kutumia hoja za nguvu havitasaidia, badala yake tunahitaji nguvu za hoja zitakazowaelimisha na kuwashawishi wananchi wa Mtwara katika maeneo yafuatayo:
-Ni vigezo gani viltumika kufikia maamuzi ya kujenga bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar Es Salaam? Kwa nini mtambo wa kuzalisha umeme usijengwe Mtwara na kusambazwa kuja Dar Es Salaam? Je mchanganuo wa gharama ukoje?
-Je upatikanaji wa Gesi hii utakuwa na manufaa gani kwa wananchi wa eneo husika? Je kutakuwa na viwanda vya kusindika gesi vitakavyojengwa huko Mtwara?
-Je mikoa inayozalisha itapata asilimia ya mapato ya gesi inayozalishwa katika eneo hilo?
Je, ajira ngapi zitakazozalishwa na sekta hii, na asilimia ngapi ya ajira zitakuwa kwa ajili Wa wakazi wa eneo hili?

Ushauri wangu ni kwamba suala hili linapaswa kushughulikiwa mapema na kwa haraka wakati likiwa bado ni kipele, Tatizo likishakuwa jipu au kansa, gharama za kulishughulikia zitakuwa kubwa sana.

Wananchi kuhoji si dhambi wala uhaini. Uelewa wa wananchi umekuwa, wanahitaji kushirikishwa na kupewa majibu ya kina. Tuzibe ufa sasa hivi lasivyo tutajenga ukuta.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized and tagged , , . Bookmark the permalink.

One Response to Changamoto ya Gesi ya Mtwara ishughulikiwe haraka

  1. Pingback: Utatuzi wa uvunaji wa gesi Mtwara bado kitendawili. Chanzo ni nini? | Faustine's Baraza

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s