Shughuli za Jimbo mwezi Agosti na Septemba 2012

1-18.08.2012 
Bungeni
26.08.2012 
Zoezi la Sensa
01-09.2012 
Zoezi la Sensa linaendelea
11.09.2012 
Nilikuwa Mgeni Rasmi mahafali ya shule ya msingi Loius Frey Amigo, Tungi, Kigamboni.
 12.09.2012 
Nilishiriki ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kilwa na ujenzi wa daraja la Kigamboni uliofanywa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt John Magufuli
13.09.2012
Nilitembelea eneo la ulipaji fidia za mlipuko wa mabomu ya Mbagala huko Mbagala Kuu. 
Vilevile siku hiyo hiyo niliongea na viongozi wa baraza la kata la Mbagala Kuu kujua changamoto za kazi zinazowakabili.
15.09.2012 
Nilifanya maongezi na vijana wahitimu wa vyuo vikuu wanaoishi Kigamboni. Tulijadili changamoto za ajira na fursa zilizopo za ajira mbadala na shughuli za ujasiriliamali. 
Siku hiyo hiyo, nilizindua kikundi cha VICOBA cha Mchikichini Modern Group kilichopo Kimbangulile. Niligharamia mafunzo ya miezi mitatu kuhusu uendeshaji wa shughuli za vikundi, ujasiriamali na VICOBA.
19.09.2012 
Nilishiriki kwenye sherehe za uzinduzi wa mradi wa Mabasi yaendayo kasi (DART) kwenye viwanja vya Jangwani uliofanywa na Mhe. Rais Jakaya Kikwete.
20.09.2012 
Nilishiriki kwenye sherehe ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni uliofanywa na Mhe Rais Jakaya Kikwete.
21.09.2012 
Nilitembelea miundombinu iliyoharibika kwa mafuriko ikiwa ni pamoja na daraja la Mangaya. Nilikagua mradi wa maji wa Kingugi. 
Nilifanya mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kata ya Kiburugwa.
Jioni nilifanya mkutano wa hadhara wa wananchi kujadili kero na changamoto zinazowakabili.
22.09.2012 
Mgeni Rasmi mahafali ya Shule ya Sekondari Charambe na kuzindua kisima cha maji na huduma iliyogharamiwa kupitia mfuko wa Jimbo. 
Vilevile nilifanya ziara ya kukagua miundombinu ya daraja la Mwanamtoti, Kijichi na barabara za Kijichi.
Siku hiyo hiyo nilishiriki kwenye harambee kwa ajili ya madawati na huduma za umeme kwenye shule ya Toangoma. Jumla ya Tsh 10 zilipatikana.
23.09.2012 
Nilikuwa Mgeni Rasmi harambee ya kwaya ya kigango cha kanisa katoliki Gezaulole, Somangila.
26.09.2012 
Nilifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara na madaraja kata ya Pemba Mnazi nikiwa na Meneja wa Tanroads na injinia wa Manispaa. 
Siku hiyo hiyo nilitembelea shamba la Amadori na kufanya mkutano na wananchi wenye mgogoro na mwekezaji huyu.
27.09.2012 
Nilikuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali ya Shule ya Sekondari ya Kisota, Mjimwema.
28.09.2012 
Mkutano na wahanga wanaodai fidia ya nyumba zilizobomolewa kupisha Upanuzi wa barabara ya Kilwa mwaka 2002.
29.09.2012 
Nilishiriki kwenye uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya Wilaya waCCM.
30.09.2012 
Nilikuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali ya Shule ya msingi ya SDA Mikwambe, Toangoma.

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

One Response to Shughuli za Jimbo mwezi Agosti na Septemba 2012

  1. Ally Yunus. says:

    Hello,Each new day is an opportunity to start all over again,to clarify your vision take a big step and make our dreams come through coz betrayal teaches us we can survive anything,all the things we thought we couldn’t handle we can so keep it up, MP and make us proud to have you we looking forward for a new kigamboni and plz keep us update cheers.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s