Nyumba za NHC na NSSF Kigamboni, Dar Es Salaam

20120511-212926.jpg

20120511-212943.jpg

20120511-213000.jpg

20120511-213144.jpg

20120511-213203.jpg

20120511-213259.jpg
Picha tatu za juu ni za NHC na tatu za chini ni za NSSF.

Juzi na jana nilipata fursa ya kutembelea miradi ya nyumba zinazojengwa na shirika la nyumba Tanzania (NHC) na NSSF jimboni kwangu Kigamboni.

NHC ina mpango wa kujenga nyumba zipatazo 200 na NSSF ina mpango wa kujenga nyumba 300 katika awamu kwa kwanza. Nyumba hizi ni za aina tofauti na zina vyumba kati ya 2-4.

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko toka kwa wananchi kuwa nyumba za bei nafuu (affordable houses) bado si rahisi kwa mwananchi wa kipato cha kati na chini. Bei ya nyumba mpya za NHC hivi karibuni zimekuwa ni zaidi ya TSh 100 millioni kila moja. Bei hii inalalamikiwa kuwa ni kubwa sana kwa mlalahoi.

Katika mradi huu wa Kigamboni, NHC ina mpango wa kuuza nyumba zake kati ya TSh 30-40 millioni kutegemea na ukubwa. Sikuweza kupata bei za nyumba za NSSF.

Pamoja na miradi hii mizuri itakayopendezesha Jimbo la Kigamboni, nyumba hizi zinaweza kununuliwa kwa matajiri wachache kutokana na bei kuwa kubwa. Kuna umuhimu wa kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini na kati kupata mikopo ya muda mrefu itakayowawezesha kununua nyumba hizi.

Kwa watanzania walio nje ya nchi, hii ni fursa nzuri ya kununua nyumba, itumieni.

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

54 Responses to Nyumba za NHC na NSSF Kigamboni, Dar Es Salaam

  1. Aysha S Mzee says:

    Where can we get the forms and is it possible to see the house

    Like

  2. malik says:

    je tutapataje form ?

    Like

  3. Aysha S Mzee says:

    Tutashukuru sana tukipewa taarifa mapema nasi tununue hizo nyumba ama sivyo wachache watanunua na kuzipangisha kwa bei wanayoitaka au kuziuza ahsante

    Like

  4. Aysha S Mzee says:

    When can we see the houses

    Like

  5. Patrick Nhigula says:

    Faustine, landscaping? $62,500 ? in Tanzania, Kigamboni and incomplete house inventory? I hope this is not another housing bubble in Tanzania. They need to invest in landscaping and having home owners association (HOA) declaration law pass in Bunge to control housing and neighborhood. If the government is willing to invest in people retirement monies like that I think they have to form a bill that will help to protect people investment.HOA helps to maintain the landscaping, security, and others things that will keep up with cost associate with running the neighborhood…..

    Like

  6. tetera mamuya says:

    Mh. Tufahamisheni na ss tu nunue

    Like

  7. Subira says:

    Habari Dr Faustine, mimi naomba taarifa kuhusu Kigamboni, nina kibanda changu nilijenga siku nyingi katika eneo langu huko Kigamboni. Bahati mbaya wakati wa upimaji wa viwanja vya Kibada eneo langu halikubahatika kupimwa na kuingia kwenye ramani, yaani ni barabara tu ndio inayotenganisha eneo langu na eneo la lilipoishia viwanja vilivyopimwa vya Kibada.

    Sasa baadae nikasikia kuwa serikali imezuia uendelezaji wa maeneo huko Kigamboni kwa hiyo nikaacha kujenga wala kuliendeleza eneo langu ambalo nilikuwa na mpango wa kulipima na kujenga nyumba ya kuishi na watoto wangu. Nina maswali yafuatayo:-

    1. Je hiyo amri ya kusitisha uendelezaji wa maeneo bado ipo?
    2. Je ninaweza kuomba kupimiwa eneo langu nikalipia gharama?
    3. Na je serikali ina mpango gani kwa sie ambao tumekaa tunasubiri kuhusu maeneo yetu?
    Kwa mfano mimi niko masomoni na nilitegemea nijenge hapo nipate pa kuishi na watoto wangu, sasa kutokana na usitishwaji huo sijafanya lolote na laiti ningelipimiwa au kupima eneo langu kipindi cha miaka 2 iliyopita nikajenga, gharama zake za ujenzi zisingekuwa kubwa kama ilivyo sasa, yaani ningeweza kuafford kujenga; sasa gharama za ujenzi zimeongezeka, je serikali ina mpango wowote wa kutulipa fidia kucompasate hii different cost inayotokana na muda?

    4. Hapo naona wenye uwezo (mashirika) wameruhusiwa kujenga; naomba unipe ufafanuzi ni maeneo yapi yamekatazwa na yepi yameruhusiwa kujengwa na kuendelezwa?

    5. Na hilo eneo langu ambalo nimekatwa kuliendeleza nilifanye nini sasa wakati kimfaacho mtu ni chake? Litanisaidia vipi hilo eneo kipindi hiki? Maana hilo eneo langu lilikuwa sehemu ya shamba langu nikijilimia mboga mboga miaka mingi nikisitiri na wanangu.

    Ni mimi muathirika wa mambo yanayotukia Kigamboni

    Mrs. S Feruz

    Like

  8. Bhavini says:

    hii nikointrested na nyumba hizi naomba uni inform mki anza ku uzza

    Like

  9. michael john says:

    Tunaomba utupatie utaribu wa jinsi gani tutapata hizo fomu na wakati gani?

    Like

  10. mama B says:

    nami nataka form jamani Faustine,tafadhali usiache kutujuza mara zitakapotoka

    Like

  11. beth joan says:

    is it possible to view the inside look of the house and the finishing.

    Like

  12. Emmanuel says:

    gharama zake ni ngapi?

    Like

  13. abubakar mgaya says:

    fomu za hizo nyumba zinatolewa wapi ili tuweze kujaza na naomba kujua hizo nyumba gharama zake ni shilingi ngapi.

    Like

  14. Jumanne Hassan Mlimakala says:

    Mimi naombakujua jisiyamaripo ya nyumba hizo Mlimakala-818041616749 nataka nyumba za NSSF

    Like

  15. Bakari Kidasi says:

    How can i get one of NSSF? Please inform me as soon as possible so that i can get myself prepared!

    Like

  16. Magige Julius J says:

    Tafadhari naomba unijulishe kama mna nyumba za kupanga na gharama zake zikoje? kwa mikoa ya Dar na Moro

    Like

  17. jumanne mpeta says:

    naomba nijue bei za chini zaidi kati za nyumba hizo za kibada

    Like

  18. faustine says:

    Jamani nyumba zote za NHC kibada zimeshauzwa! Form ziko katika website ya nhc. Dot.com alieko karibu atakuelekeza

    Like

  19. Anderson Mwaga says:

    Nahitaji kupata ramani ya nyumba ya bei nafuu

    Like

  20. gulzar khimji says:

    i am interested can you please contact me. thanks

    Like

  21. isack mboya says:

    HBR? FORM ZIMETOKA KWA AJILI YA KUNUNUA NYUMBA ZA NHC?

    Like

  22. asia top says:

    habari yako ndugu faustine mimi nauliza je hawazipangishi hizi nyumba?na kama wanapangisha ni sh ngapi?maana tusioweza kununua tupange.

    Like

  23. Mariah says:

    Ahsante Mheshimiwa kwa taarifa nzuri. Naomba kujua mpaka leo bado hazijaanza kuuzwa?

    Like

  24. Prakash Nadiadhara says:

    Hello sir, I would be very please if you can tell me when you are going to distribute the forms.
    i’m very much interested to get house and would like to know rates of the house and procedure as well.Thanx in advance.

    Like

  25. Jacq says:

    wanaanza lini tena kuuza ?

    Like

  26. Prakash Nadiadhara says:

    sir, prices are too high for middle class family to purchase only business person can afford i hope so.But person who is earning less then 500,000/= per month do you think they can afford this houses? I don’t think so.
    please work out again these house prices so, middle class family can afford to buy specially for Tanzanian Citizen. Please do see into this matter and let us know. Thank you.
    regads from local citizen Prakash.

    Like

    • Mariah M. Hamson says:

      Dear Faustine,

      Ahsante sana kwa taarifa nzuri na muhimu.

      Tafadhali endelea kutujuza.

      Mariah/TTB
      ===

      Like

  27. ALLY NYAU says:

    mimi Ally Nyau wa Arusha naombeni form zenu zikiwa tayari mnitumie .

    Like

  28. lau says:

    Habari.za kazi wadungu.ninashangazwa sana kuona number zinakuwa NA bei kuliko ninapo ishi hivi sasa’ mawazo ni manzuri kabisa yakujenga katika hali ya mpangilio.ninamanisha kila mtu kujulikana anaishi wapi Hayo ni mawazo manzuri sana ILA bei ndiyo kubwa tens mno from Lau.

    Like

    • Lucas lyimo says:

      Mimi nimesomea umeme wa majumbani VETA Chang’ombe na kupata cheti cha daraja la kwanza. nitawezaje kujiunga nanyi?
      contact zangu ni 0657300144

      Like

  29. steven dastan shewiyo says:

    kweli nyumba ninzur nimependa san naweza kupata mawasiliano namba yangu 0762051991 /0715423451 nataka nyumba namba zangu izo pamoja na mkopo jamani naomben sana???????

    Like

  30. moza mustafa says:

    Habari ..jaman nitapata je form za kununua hizo nyumba naomba nijibu

    Like

  31. elisia sixbert says:

    naomba kujua bei ya nyumba yenye vyumba vi4. na vigezo au mashart.

    Like

  32. Humphrey Msechu says:

    habari za kazi….nyumba ni nzuri na nimezipenda sana ,nianweza kuzipata kwa sasa au mwaka huu?……

    Like

  33. Magreth says:

    Habari. Naomba kufahamu utaratibu wa ujenzi mpya kama mna mpango wa kujenga karatu au arusha eneo gani na bei zake zitakuwaje kwa maisha ya mtanzania wa kawaida. Mag

    Like

Leave a comment