Utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano

20120508-114124.jpg
Leo asubuhi nimeshiriki kwenye semina iliyoandaliwa na wakala wa vizazi na vifo (RITA). Lengo la semina hii ilikuwa kuhamasisha wadau kuhusu zoezi la majaribio la kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwenye kata 14 za majimbo ya Kigamboni na Temeke.

Hivi sasa ni asilimia 14 ya watoto chini ya miaka mitano wamesajiliwa na ni asilimia 6 tu ambao wana vyeti vya kuzaliwa. Tanzania ndio nchi pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashiriki yenye idadi ndogo ya usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano.

Nimefurahia mikakati ambayo RITA inayo ili kuondokana na tatizo hili.

RITA imepanga kufanya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa mitano baada ya zoezi la majaribio katika Wilaya ya Temeke. Majaribio haya yanalenga kufanya tathmini ya makakati mbalimbali ya maboresho wanayotarajia kuyafanya.

Ili kuondokana na ukiritimba uliopo RITA imepanga kupanua wigo wa utoaji wa huduma hii. Wanatarajia watumishi wa Afya kutoa vyeti vya kuzaliwa kwenye zahanati, vituo vya Afya na mahospitalini. Kwa watoto wanaozaliwa nje ya mfumo wa hospitali, wakunga, watendaji wa vijiji, mitaa na kata watahusika.

Vilevile RITA ina mpango wa kufanya maboresho katika utumiaji wa teknolojia ya mtandao na simu kutoka vijijini hadi makao makuu ya RITA ili kurahisisha upatikanaji na utunzaji wa taarifa.

Nawapongeza RITA kwa maboresho haya makubwa ambayo yanatarajia kuyafanya na ninaahidi kuwapa ushirikiano wangu ili watoto chini ya miaka mitano katika Jimbo la Kigamboni wanasajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

3 Responses to Utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano

  1. Patrick Nhigula (PhD), Epidemiology Consultant:PNN Consulting Firm says:

    Dr. Faustine, State or National Vital registration system is needed in Tanzania. Health dept. should include births, dealth, marriages, divorces, etc…this effort will help to measure health status of population

    Like

  2. naomba kufahamu kama RITA ina system (database) yoyote ya kuhifadhi taarifa za vifo,vizazi ,ndoa na talaka kwa sasa. ni vema kama utani email via, aididrash20@yahoo.com

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s