Mgomo wa madaktari

Hali ya utoaji wa huduma za afya nchini umezidi kudorora kutokana na  mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa nchini Tanzania. Agizo la Waziri Mkuu kuwataka madaktari kurejea kazini limeonekana kupuuzwa. Madaktari wamekuwa wakiripoti mahospitalini pasipo kufanya kazi au kutoa huduma.

Athari za mgomo huu ni pamoja na kusimama kwa operesheni zisizo la dharura (elective surgeries), kliniki za kawaida na hata huduma za dharura katika baadhi ya hospitali. Baadhi ya mawodi kwenye mahospitali zimebakia tupu baada ya wagonjwa kuondolewa na ndugu zao. Sijapata takwimu za wagonjwa waliofariki tangu sakata hili kuanza, ila nina taarifa za vifo vya wagonjwa watatu waliofariki katika hospitali mbalimbali kutokana na kukosa huduma za matibabu katika kipindi hiki cha mgomo.

Taarifa nilizonazo ni kwamba Serikali imepeleka madaktari 15 kutoka kwenye Jeshi la Wananchi kwenda kwenye hospitali ya Muhimbili kutoa huduma za dharura. Idadi hii ndogo sana kutosheleza mahitaji ya hospitali hii. Madaktari waliogoma ni wengi zaidi hawa. Hata hivyo inaripotiwa kuwa madaktari hawa walikuwa wanapata ushirikiano mdogo kutoka kwa manesi na wahudumu waliokuwepo. Kimsingi hali ya utoaji wa huduma bado ni mbaya.

Leo katika kikao cha Bunge, Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Zitto Kabwe alitoa hoja Bungeni kuitaka Serikali itoe taarifa rasmi kuhusu mgomo wa madaktari. Serikali inatarajia kufanya hivyo kesho asubuhi.

Pamoja na mgomo kuendelea pande zote zinazohusika na mgomo huu zimekuwa zikitoa kauli kwamba ziko tayari kufanya majadiliano, lakini kwa bahati mbaya sana, hakuna aliye tayari kuanzisha mchakato huu.

Kama nilivyosema hapo awali, mgomo huu usingekuwa mkubwa kiasi hii kama matatizo ya madaktari waliokuwa kwenye mazoezi (interns) yangeshughulikiwa mapema, kwa ukamilifu na pasipo kuwaadhibu kwa kudai haki zao za msingi.

Narudia rai yangu ya kuitaka Serikali kutumia hekima na busara katika kulishughulikia suala hili, kamwe amri na vitisho havitarejesha hali ya utoaji wa huduma katika hali ya kawaida. Ni vyema Serikali ikawa ya kwanza kuwaita tena mezani madaktari na kujadiliana nao. Ni dhahiri kuwa madai yote hayawezi kutekelezwa kwa wakati mmoja, lakini kwa njia ya majadiliano naamini pande zote zinaweza kufikia muafaka.

Mwisho, wananchi wanataabika, wananchi wanasumbuka na baadhi ya wananchi wakubwa kwa wadogo wamepoteza maisha kwa kukosa huduma. Sasa si muda wa kulumbana wala kushutumiana, bali ni muda wa kukaa mezani na kufikia suluhu.

Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania

 

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

One Response to Mgomo wa madaktari

 1. Matgo says:

  Thanks for this information Dr. Faustine. All you say is absolutely true, and I also respect your take onto what should be the next step. As a stakeholder in the health sector and so do you, improving the quality and safety of health services in this country and wherever else, requires meeting the needs and expectations of both internal [healthcare workers] and external [patients and community] customers. These needs and expectations are variable but at the end of the day they are all determinant factors for success.

  My analysis of this situation, doctors are for the first time in history demanding for both internal and external customers rights, expectations and needs. I am a bit disappointed by the breeze of the discussion in the sense that everyone is so focused on that doctors should return as the as the government should be addressing their needs. One could argue that this are possible, but think about hepatitis B vaccine – such a crucial but affordable intervention. Currently the Ministry is not providing for this and it is truly unacceptable. What about medical insurance for doctors? In several occasions I have been approached by colleagues that we make a contribution for fellow doctors who are admitted at Muhimbili Orthopedic Institute and other private hospital, and yet this are the key provider of the service in the country. I can not over-emphasize how the wages are a total mismatch with what these individuals do bearing in mind current inflation rates and the like.

  The external ones are more important and I bet if the community could have understood about this, may be they could be the ones denying to go to facilities. These doctors have been complaining about lack of infrastructure, materials, supplies and equipment, factors of which truly compromise the safety and quality of the services offered to patients albeit doctors presence in the facilities.

  There are some anecdotal reports on the lack of stuff listed hereunder in a number of reputable hospitals in the country
  – Lack or non-functional sterilization facilities [meaning that patients can end up acquiring preventable infections during the course of surgeries and other procedures]
  – Lack or inadequate running water and lack of water taps in the facilities [we all know that hand hygiene is the single cheap but efficient and effective intervention]
  – Lack of incinerators [meaning that the waste from hospitals get access to the community un-checked, a situation that leads into transmission of infections to the naive community]
  – Inconsistent power supply in hospitals
  – Lack of maintenance of various equipment rendering hospitals “equipmentless”

  These are just examples, but my point is I am not seeing a clear strategy in trying to address these issues, and it is high time that the government take care of the internal clients needs and promptly work together in addressing the external clients needs starting with the most life-threatening ones. There are people in the country who could work with the government in coming up with solutions if given opportunity.

  I submit

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s