Kifo cha Bw Lilla Hussein: Haki Itendeke

Leo nimepokea taarifa ya kushtusha kuwa watu wanaotuhumiwa kwa mauaji wa kijana mmoja wa eneo la Mjimwema, Kigamboni Bw Lilla Hussein, wameachiwa huru.

Bw Salim Nathoo(Chipata), Bw Bhushan Mathkar na Bw John Mkwanjiombi waliachiwa huru baada ya mwendesha mashtaka wa Serikali (DPP) kutoonyesha nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kuachiwa kwa watuhumiwa hawa kumewasikitisha wanakigamboni na kuleta hisia mbaya kuwa sheria imepindishwa kuleta unafuu kwa matajiri na kuwagandamiza maskini.

Mauaji ya Lilla Hussein yalisababisha vurugu kubwa katika jamii ya Mjimwema. Ilibidi mimi na viongozi wa Serikali ya Mtaa kufanya kazi ya ziada ya kuwasihi wananchi kupunguza hasira na kuviachia vyombo vya dola kufanya kazi yake. Kwa bahati mbaya ushiriki wa vyombo vya dola haukuwa mzuri na hali iliyopelekea kuihisiwa kuwa vilikuwa vinampendelea mwekezaji kuliko maslahi ya mwananchi aliyeuwawa kikatili. Kwa bahati mbaya hakuna kiongozi yoyote wa Serikali aliyekwenda kuwapa pole wafiwa. Lakini hivi majuzi alipokufa mama wa kichina Serikali ilishiriki kwenye mazishi na kuwasaka kwa udi na uvumba watuhumiwa wa mauaji.

Wananchi wanajiuliza kwa nini wageni wanakuwa na haki zaidi mbele ya sheria kuliko wenyeji? Kwa nini wananchi wanyanyaswe na kuuwawa kikatili katika nchi yao? Wananchi waende wapi kudai haki yao?

Uamuzi wa DPP wa kuondoa kesi mahakamani kabla ya kusikilizwa ni wa kusikitisha. Haukuzingatia maslahi ya umma wala kauli ya marehemu ambayo aliwataja waliomfanyia tukio hilo baya kabla ya kukata roho.Uamuzi huu unaleta hisia ya rushwa na upendeleo kwa wageni kuliko wazawa.

Wananchi wa Kigamboni wangependa kuona kesi hii inarudishwa tena mahakamani ili haki itendeke.  Pili, Serikali ionekane inalinda maslahi ya wananchi wake kuliko ya wageni. Tabia ya kukamata na kuwaachia wageni wanaofanya makosa nchini haileti taswira nzuri mbele ya jamii. Binafsi jambo hili limenisikitisha sana na nimeshaanza kulifuatilia.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

3 Responses to Kifo cha Bw Lilla Hussein: Haki Itendeke

 1. Tanganyikan says:

  Doctor, Kama mwananchi wa kawaida naumizwa sana na hiki kitu. Kinafanya mwananchi wa kawaida anajihisi hana haki mbele ya matajiri na mtu yeyote mwenye hela nchi hii. Hofu yangu itafikia wakati likitokea tukio kama hili wananchi wataamua kujichukulia sheria mikononi na polisi watakapofika eneo la tukio watakuta maiti tu.

  Hii sio sahihi kabisa.. kwa hiyo damu ya mtu imepotea bure tu? Ina maana ilikuwa ni haki yake kupoteza maisha? Kama muwakilishi wao nina uhakika una sauti ya kuweza kwenda kwa mwendesha mashtaka na kumueleza kuhusu maoni ya wakazi wa Kigamboni na wananchi kwa ujumla. Tunapoteza imani na vyombo vyetu vyenye kazi ya kusimamaia dola.

  Like

 2. bway says:

  chomeni hiyo hotel watu wa kigamboni hii ni dharau

  Like

 3. M says:

  Kumbe waliotaka kuichoma moto ile hoteli wakua sahihi kabisa….

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s