Je CCM imtambulishe mgombea urais ajaye sasa?

Ni mwaka mmoja tu tangu nchi yetu ifanye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2010, lakini tayari baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na baadhi ya wananchi wameanza kuangalia nani atakayesimama kwa tiketi ya urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015.

Leo katika mizunguko yangu ya kila siku, nimekutana na wananchi ambao wanakitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimwandae na ikiwezana kumtaja au kumtambulisha mgombea wake wa urais ajaye mapema. Wadau hawa walidai kuwa hali ya sintofahamu inaleta hali ya kuyumba (instability) katika nyanja za fedha, uwekezaji  na hata ndani ya chama na Serikali.

Hoja hii ilifanya nifanye tafakari kidogo kuhusiana na suala hili. Je ni busara kwa CCM kutangaza au kumtambulisha mgombea sasa hivi? Nini faida na hasara ya kufanya hivyo?

Faida za kumtambulisha mgombea mapema.

  1. Itasaidia kupunguza kasi ya makundi yanayowania urais na hivyo kuelekeza nguvu kwa mgombea mtarajiwa.
  2. Itasaidia kufanya hali ya kisiasa kuwa shwari (Political stability). Hivi sasa tumekuwa tukishuhudiana mivutano na malumbano ya kisiasa ndani ya chama na jumuiya zake. Imefikia hatua ya makundi kuzushiana vifo na tuhuma nyingine zisizofaa.
  3. Itaipa CCM muda wa kumuandaa (Groom) mgombea huyo na kumuuza kwa wanachama na wananchi.
  4. Itatoa nafasi kwa CCM na Serikali yake kuelekeza nguvu na mawazo yake katika utekelezaji wa ilani na kuleta maendeleo kwa wananchi. Sasa hivi mambo ya siasa yamechukuwa kipaumbele kuliko masuala ya maendeleo.

Hasara za kumtambulisha mgombea mapema

  1. Itatoa muda wa kutosha kwa makundi hasimu na vyama vya upinzani kumbomoa, kumtengenezea kashfa au kutafuta visa vya kumharibia mgombea huyo.
  2. Makundi yaliyozidiwa nguvu yanaweza kumhujumu mgombea ili ashindwe kwenye uchaguzi.
  3. Mgombea atakuwa anaangaliwa na kuchunguzwa kwa makini na wananchi. Hivyo kuna hatari ya mgombea kupoteza mvuto kwa wananchi kabla ya uchaguzi huo.
  4. Mgombea husika anaweza kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo akiogopa kupata kashfa au kuwaudhi wananchi.

Tuna miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine. Huu si muda  mrefu. Kuna kila umuhimu kwa CCM kuanza kujipanga kwa kuangalia mfumo mzuri wa kupata mgombea wa urais. Wananchi wengi wataka kuona Rais ajaye awe ni mtu wa kuweza kuwapa wananchi matumaini, awe ni mtu wa kuthubutu kufanya maamuzi magumu, awe ni mtu atakayeweza kukemea rushwa na ufujaji wa mali za umma, awe ni mtu atakayelinda rasilmali za wananchi ili ziweze kutumika kwa wananchi wote, awe ni mtu mwenye kuguswa na umaskini wa watanzania walio wengi na mwisho awe ni mtu ambaye anaweza kuwafikia na kukubalika na vijana ambao kwa sasa ni takribani asilimia 60-70% ya taifa hili na wanaweza kubadili mwelekeo wa matokeo kutokana na wingi wao.

Je ni busara kwa CCM kumtambulisha mgombea wake ajaye mapema? Nini maoni yako kuhusu hoja hii?

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s