Nini baada ya uchaguzi wa Igunga?

Uchaguzi mdogo uliofanyika Igunga siku ya Jumapili 2/10/2011 ndio uliokuwa ukisikika katika vyombo vya habari kwa takribani mwezi mmoja sasa. Ingawa kulikuwa na mambo mengine makubwa ya kitaifa, mambo hayo hayakupewa nafasi katika vyombo vyetu vya habari. Vyombo vyetu vya habari vina matatizo ya kuangalia zaidi stori zinazouza magazeti badala ya kuangalia pia zile zenye kuelimisha na kupasha habari umma.

Sasa uchaguzi umeisha walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa. Ni muda muafaka sasa kwa vyama husika kufanya tafakari ya matokeo hayo. Nini kilitokea, nini kilipaswa kufanyika na vyama hivi vinajipanga vipi kwa chaguzi zijazo.

Baadhi ya mambo ambayo yametokea hapa katikati lakini kutokana na ushabiki uliokuwepo juu ya uchaguzi huu mdogo hayakuwepa nafasi ni pamoja na:

  1. Mchakato wa Katiba mpya-Mchakato wa kupata katiba mpya unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni mwezi Novemba. Lakini kwa bahati mbaya suala hili haliongelewi tena pamoja na umuhimu wake. Wanaharakati, wanasiasa na wadau wengine wamekuwa kimya.
  2. Elimu-Vijana wa kidato cha nne wameanza mitihani yao ya mwisho jana. Vilevile Serikali imetoa taarifa ya kurejesha mitihani ya kidato cha pili. Taarifa hii nzuri nayo imepita kimya kimya. Hali kadhalika kuna suala la baadhi ya wanafunzi wanaoingia chuo kikuu kukosa mikopo toka bodi ya mikopo (HELSB).
  3. Malipo ya Dowans-Hivi majuzi Mahakama Kuu iliridhia hukumu ya malipo  ya Dowans kusajiliwa ikiwa ni hatua muhimu kabla ya malipo kufanyika. Wako wapi wanaharakati na waliokuwa wanalipigia sana kelele sana suala hili?
  4. Chenji ya Rada-Tulipokea taarifa njema ya kurejeshwa kwa chenji ya rada nchini. Hakuna anayekumbushia uwajibikaji wa wale waliosababisha tukapoteza fedha hizi. Au kwa sababu fedha zimerudi makosa yamefutika? Vyombo vya habari vina wajibu wa kukumbushia mambo haya.

Nasubiria kwa hamu kuona mwelekeo wa vyombo vya habari na wananchi katika muda uliobaki wa mwezi huu.

Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania

 

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s