Ajali ya meli Zanzibar na ufinyu wa habari

Awali ya yote napenda kuwapa pole wahanga wa ajali na wafiwa wote wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyozama huko Zanzibar usiku wa kuamkia jana.

Napenda kuvipongeza vyombo vya dola na watu binafsi waliojitokeza na kukoa wahanga na pia kuopoa maiti. Wamefanya kazi nzuri na kwa kujituma.

Kuna tatizo ambalo nimeliona kwa upande wa upatikanaji habari. Pamoja na ajali hii kuwa kubwa, hakukuwa na upatikanaji wa habari za uhakika. Wananchi walitegemea zaidi vyombo vya habari vya nje kuwahabarisha. Huu ni udhaifu mkubwa. Mfumo wa habari jamii kama blogs, Twitter, Facebook vilifanya kazi nzuri za kuziba mapengo ya habari.

Vyombo vya habari kama shirika la utangazaji la taifa (TBC) vilipaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha jamii na pia kuwa chanzo cha news feed kwa mashirika ya habari ya nje. TBC imepoteza nafasi muhimu na adimu ya kujitangaza na kujipatia.

Ajali hii imedhihirisha mapungufu ya kiutawala ya shirikia hili, njia zinazotumika katika kutafuta habari, mtandao wa upatikanaji habari na upimaji wa umuhimu wa habari. Katika ajali hii TBC ilikuwa kwenye usingizi wa pono na bado wapo usingizini.

Pamoja na changamoto za ufinyu za bajeti TBC bado ina wajibu kwa wananchi na Taifa hili. Utendaji wa TBC kwa siku ya jana na leo umewaangusha wananchi. Kuna kila umuhimu wa kujipanga upya.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

2 Responses to Ajali ya meli Zanzibar na ufinyu wa habari

  1. Pingback: #ZanzibarBoatAccident and the Tanzanian media – failure all round? « mtega

  2. Pingback: The Tanzanian media has had a bad crisis « mtega

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s