Rites na uwekezaji usio makini

Leo nimesoma kwa masikitiko taarifa kwenye gazeti la Guardian on Sunday kuhusu kampuni ya wawekezaji wa India katika reli yetu Rites kulipwa kiasi cha Tsh 30 billion (USD 20 million) kama malipo ya kukatisha mkataba na wao.

Ni jambo la kusikitisha sana na lenye hasara kubwa kwa nchi kama yetu yenye uchumi mchanga.

Kwa fedha hii tungeweza kufanya mengi ya maana katika kuboresha huduma za elimu, maji, umeme, afya au miundombinu.

Uwekezaji huu wa Rites katika shirika letu la reli umekuwa unapigiwa kelele tangu mwanzo. Badala ya kuimarisha , kampuni hii ya India ilikuwa likinyonya na kulididimiza shirika hili. Uwekezaji wa kibabaishaji kama huu unapaswa kukomeshwa hauna tija wala manufaa kwa nchi yetu.

Vilevile, ingawa mimi si mtaalamu wa masuala ya sheria, ni dhahiri mkataba kati ya Serikali na wawekezaji hawa ulikuwa na mapungufu makubwa.

Kama kweli hatukuyaona mapungufu haya, basi ni dhahiri kwamba baadhi yetu tumeshiriki katika kuliangamiza shirika hili kwa maslahi binafsi. Sitaki kuamini kuwa wataalamu wa sheria hawakuyaona haya.

Nadhani imefika wakati sasa kutokana na mapungufu haya, kuna haja ya mikataba ya uwekezaji kuridhiwa na Bunge.
Rasilmali za nchi hii ni za watanzania wote na vizazi vyetu vijavyo. Hakuna mantiki ya kufanya mikataba kuwa siri wala maamuzi haya makubwa kufanywa na watu wachache. Ifike sasa wakati maamuzi yanayowagusa wananchi yafanywe na wawakilishi wa wananchi.

Nawatakia Sikukuu njema ya Pasaka na Muungano.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s