Suala la katiba mpya limeishia wapi?

Mwishoni mwa mwaka jana na mapema mwaka huu suala la katiba lilikuwa ajenda kuu katika jamii ya watanzania. Vyombo vya habari, mijadala mbali mbali na vyama vya siasa vililishikia bango suala hili na ikafika sehemu kukawa na maandamano ya kudai katiba mpya.

Cha kushangaza kuwa ajenda hii kwa sasa haiongelewi tena. Ilikuja kufunikwa na ajenda ya mgao wa umeme na sasa ajenda ya Babu wa Loliondo.

Najikuta napata maswali mengi kuliko majibu.

  1. Je, ni kweli tunahitaji katiba mpya? Mbona kwa sasa suala hili haliongelewi tena?
  2. Je, inawezekana kilio tulichokuwa tunakisikia kuhusu katiba mpya kinatoka kwa kikundi wachache? Mbona umma wa watanzania hawaliongelei tena suala hili? Suala hili haliwagusi au haliwahusu kwa sasa?
  3. Je, suala hili limesahaulika?

Nasema hivi kwa sababu suala hili haliongelewi wala kugusiwa kabisa katika mijadala inayoendelea kuanzia kwenye vijiwe vya kahawa hadi kwenye ngazi za maamuzi. Hali hii inapelekea kuhisi kuwa sisi kama watanzania tusahau haraka sana au ni watu wenye ajenda za msimu.

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

One Response to Suala la katiba mpya limeishia wapi?

  1. Baraka Mollely says:

    jamani hawa wabunge wana2tania hapo bungeni! haiwezekani muda wote wapo wanagombana hapo bungeni bila kufikia miada!

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s