Babu wa Loliondo

Kwa takribani wiki tatu sasa vyombo vyote vya habari pamoja na gumzo kwenye vijiwe mbali mbali vimekuwa kuhusu tiba ya Babu Ambikile Mwasapile wa huko Loliondo.

Na mimi kama mbunge nimekuwa nikipata shida kubwa toka kwa wapigakura wangu wakitaka nifanye utaratibu wa kupeleka baadhi ya wagonjwa jimboni kwangu huko Loliondo. Wagonjwa mmoja moja na kwa makundi wamekuwa wakifurika ofisini kwangu.

Kwa upande mwingine kuna watu wanafurahia suala hili.
Suala la mgao wa umeme na kupanda kwa bei za bidhaa
haliongelewi tena. Tanesco, wizara ya nishati na madini pamoja na kamati ya bunge ya nishati na madini zimeweza kupata nafasi ya kupumua.Sasa sijui shida imeisha au kwamba watanzania tunasahau haraka.

Mimi binafsi naipa tiba miezi 2-3 kabla ya wananchi kugutuka na kujua ukweli.

Dawa hii kitaalamu ina viini vya tiba ya kifafa, presha, kisukari na kuthibiti virusi. Naamini kuwa dawa hii inaweza kuleta ahueni ya muda na sio kutibu kabisa maradhi husika.

Kuna haja ya kufanya utafiti wa kina wa dawa hii. Wataalamu wetu inabidi kuwaomba baadhi ya wagonjwa wanaoenda kwa Babu kushiriki kwenye utafiti huu. Wagonjwa hawa wapimwe na kuchunguzwa afya zao kabla ya kuanza matibabu na waendelee kupimwa na kuchunguzwa afya kwa muda baada ya kupata “Kikombe”. Majibu ya utafiti huu yatatupa ukweli kuhusu tiba hii.

Kwa sasa, tiba hii imekaa ku-imani zaidi kuliko kitaalamu.

NB: Siku hizi mbili ka-mgao ka umeme kamepungua, TANESCO wamepata “kikombe” nini?

Advertisements

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s