Mfuko wa Jimbo

Civil Society Organisations (Taasisi za kijamii) ni moja ya nguzo muhimu sana katika nchi na wana mchango mkubwa katika kuelimisha jamii na pia kukosoa Serikali, Bunge na mahakama.

Hivi majuzi nimesikia kupitia vyombo vya habari kuwa wanaharakati wamepeleka kesi mahakamani wakitaka kufutwa kwa mfuko wa jimbo.

Katika muda mfupi wa Ubunge wangu, nimeweza kutumia fedha hizo kununua madawati 500 ambayo niligawa kwa shule 10 za sekondari katika jimbo langu. Pili, nimeweza kuchangia katika ujenzi wa choo wa shule ya msingi ya Mponda ili waweze kutumia madarasa waliyojenga kwa kutumia nguvu zao wenyewe. Kwa sasa watoto wa eneo hili wanasafiri umbali wa takribani kilometa kumi kwenda shule kila siku.

Matumizi ya fedha za mfuko hayapangwi na Mbunge peke yake, kuna kamati inayokaa na kupanga matumizi ya fedha. Kwa hiyo hakuna hatari ya fedha hii kutumika vibaya. Vile vile Mbunge hashiki fedha hii mkononi.

Kwangu mimi, naona mfuko huu unamsaidia sana mbunge kuchangia shughuli za maendeleo kwenye jimbo lake.
Kwa mtazamo wangu sababu zilitolewa na wanaharakati kupinga uwepo wa mfuko huu ni hafifu sana. Nachelea kusema kuwa inawezekana sababu ya kwenda mahakamani kuna msukumo wa kisiasa.

Naheshimu sana mchango wa wanaharakati katika jamii lakini kwa hili naona wapepotoka.

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

6 Responses to Mfuko wa Jimbo

 1. Mhe. Dr. Faustine,

  Nashukuru unathamini mchango wa asasi za kiraia katika kuelimisha jamii na pia kukosoa Serikali pamoja na Bunge. Hata mimi nathamini mchango wabunge wanatoa kwa jamii haswa kuhusiana na nafasi walioyopewa kikatiba (uwakilishi, utungaji sheria na kuisimamia serikali inavyotekeleza shughuli zake). Nilifurahi uliposhinda uchaguzi jimboni kwetu (wewe ni mbunge wangu) na ninayo imani kubwa kuwa kwa kudra za mwenyezi Mungu utaifanya kazi yako vizuri.

  Nimesoma magazetini kuhusu habari za wewe kutumia fedha za mfuko wa majimbo kununulia madawati 500 kwa ajili ya shule za sekondari. Hakuna anayekataa shule zipate madawati ila ni lazima tuulize jambo moja la msingi. Ni shughuli za mbunge kutekeleza miradi ya maendeleo? Ningetegemea kwa majukumu wabunge waliyopewa kikatiba (oversight) mngeisimamia na kuishauri serikali ipasavyo ili iweze kutekeleza majukumu yake vizuri ikiwemo kutoa huduma muhimu kwa jamii kwa ufanisi, na kuiwajibisha pale inaposhindwa. Katiba yetu Ibara ya 63 na 64 inaeleza wazi hili jambo.

  Vile vile, katiba yetu Ibara ya 4 inatueleza vizuri suala la mgawanyiko wa madaraka (separation of powers). Hivyo wabunge waiachie serikali ndiyo iendelee na jukumu la kutekeleza miradi ya maendeleo.

  Nilifuatilia kwa karibu kampeni za ubunge mwaka jana. Nilichogundua cha kusikitisha ni kuwa wagobmea wengi walikuwa hawajaelewa vizuri kazi za mbunge na hili lilidhihirika wazi pale ambapo walikuwa wakitoa ahadi ambazo hazihusiani kabisa na kazi zao.

  Mhe. Faustine, naipenda sana Kigamboni kama jimbo. Siyo tu kwamba naishi Kigamboni kama kata, ninao ndugu na jamaa vijibweni, Kibada, Chamazi n.k. ambao wote wangependa mifumo iliyopo iweze kufanya kazi kwa manufaa yao haswa kwa kuwasaidia kuondokana na maisha magumu yanayowakabili. Mbunge kugawa madawati inaweza kuonekana ni jambo zuri. Ila kwa nini hatuulizi nini kilichoishinda Halamashauri (ambayo ndiyo kazi yake) kufanya hivyo?

  Mbunge akifahamu ulegevu wa mifumo ndani ya serikali, yuko katika nafasi nzuri zaidi ya kushauri wapi marekebisho yafanyike. Ndiyo maana asasi za kiraia zingependa kushirikiana nanyi ili kuhakikisha kwamba wabunge wote wana ofisi majimboni ili wawe karibu na wananchi; kuboresha mfumo wa mawasiliano katika ya wabunge na wananchi majimboni ili kuwawezesha wabunge kupata taarifa sahihi za utekelezaji wa mipango ya serikali; kumwezesha kila mbunge kuwa na wasaidizi rasmi wanaoweza kufanya utafiti, kufuatilia masuala na kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya usimamizi na ushauri kwa serikali.

  Vile vile, ningeshauri wabunge msisitize mnafunguliwa ofisi ya bajeti kwa ajili ya wabunge (parliamentary budget office). Hii ni tofauti na ile iliyopo serikalini kwa maana ya kwamba inatoa mchanganuo ‘huru’ na mbadala kwa ajili ya matumizi ya wabunge kuhusiana na masuala ya bajeti. Ofisi kama hizi ziko Kenya, Uganda, Ghana na Morocco na zimeonesha kusaidia sana na kukuza uwezo wa wabunge kuisimamia serikali.

  Kuna jaji mmoja Supreme Court ya Marekani alisema: “If the whole legislature . . . should attempt to overlap the bounds prescribed to them by the people, I, in administering the public justice of the country, will meet the united powers at my seat in this tribunal; and pointing to the Constitution will say to them here is the limit of your authority, and hither shall you go no further.”

  Kwa kifupi ni tutizame upya kikomo cha mamlaka ya mbunge kikatiba (wanajimbo wenzetu kutoelewa vizuri kikomo hicho, isiwe sababu).

  Like

 2. tahir says:

  Sem, mambo yakuanza kuangalia mifumo inafanyaje kazi will take forever na on he ground we just need the shit to be done doesn’t matter who is doing it. Nyie wasomi endeleeni kuchambua ila mimi niko na Mbunge wangu, tujenge Taifa brick by brick.

  Like

 3. Pingback: Constitutional Debate on Constituency Development Funds in Tanzania « AfriCommons Blog

 4. Tahir, ni kweli wananchi tunataka ‘action’ ya mara moja. Ila kama hatutauliza maswali ya msingi (kwa mfano kwa nini shule zimepangiwa 10,000/- kwa kila mwanafunzi lakini hazifiki kabisa au zikifika ni shillingi 390?) na kufikiri njia rahisi ni kumuomba mbunge kupitia mfuko wa majimbo atatue hayo matatizo(clogging the ineffective system even further) basi tutaendelea milele kulia kilio cha mtema kuni. Mfuko wa majimbo (ukiachilia kukinzana na katiba) ni njia inayoonekana rahisi lakini ndiyo inadhoofisha kabisa mfumo.

  Matatizo ya Tanzania yanatatuliwa kwa kurekebisha mifumo, siyo kwa kuanzisha mifumo juu ya mifumo.

  Siku wananchi wote watakapotambua kuwa matatizo ya maji, elimu, miundombinu, n.k. yanahusu mifumo mibovu (ambayo wewe na mimi tuonaogopa kukabiliana nayo maana tunaona kama ni kazi ngumu), ndipo itakuwa mwanzo wa kujikwamua na taabu za Tanzania.

  Ndugu yangu Tahir, naomba ukumbuke hilo utakapokwenda ofisi yoyote ya serikali siku za usoni ukafedheheshwa na huduma au kutopata huduma unayostahili kama mlipa kodi. Mfuko wa majimbo hapo hautakusaidia.

  Like

  • Mimi says:

   Sem umesema sahihi, mfumo mzima inabidi uangaliwe na upewe tiba badala ya kutafuta njia rahisi ya kuwafurahisha umma bila maendeleo ya muda mrefu

   Like

 5. Pingback: Mfuko wa Majimbo – Unconstitutional, or going with the grain? « mtega

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s