Kuzagaa kwa Noti feki

Ni hivi karibuni Serikali ilitangaza kubadili noti zinazotumika nchini kwa vigezo kuwa noti zilizopo zimechakaa na pia kuwa kulikuwa kuna haja ya kuwa na noti zenye vigezo bora vya usalama.

Haijapita miezi mitatu, tayari noti feki zinazofanana sana na noti mpya zimeingia mitaani na kuleta mtafaruku mkubwa. Mbaya zaidi ni kwamba noti feki hizi zimeanza kutolewa na mabenki yetu.

Wananchi wetu wengi wanaamini kuwa benki ni sehemu zinazotoa fedha halali, sasa hivi watu wameanza kuwa na mashaka makubwa kuhusiana na noti wanapokea madirishani na kwenye mashine za ATM za mabenki yetu.

Jambo la kusikitisha ni kwamba, Benki Kuu ambayo ina dhamana ya kusimamia jambo hili haijatoa tamko lolote na sijui kama wanalifanyia kazi suala hili.

Wananchi wangependa kuona hatua za haraka zinachukuliwa ili kubaini wale wote wanaohusika na matukio haya na kuchukuliwa hatua. Pili, Benki Kuu inahitaji kuzichukulia hatua benki zote zinazoshiriki katika mchezo huu mchafu.

About Dr Faustine Ndugulile

#Medical Doctor #Microbiologist # Public Health Specialist #Politician #African #Proud Tanzanian
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s